16 Desemba 2025 - 11:48
Shinikizo la Marekani kwa Baghdad; Makundi ya Muqawama: Hatufutiki kisiasa

Chanzo cha karibu na makundi ya Muqawama kilisema: “Muqawama na al-Hashd al-Shaabi pamoja na washirika wao wana angalau viti 97 bungeni, na wao ni sehemu isiyotenganishwa na mlinganyo wa kisiasa wa Iraq. Washington ilishindwa hapo awali kuyadhibiti makundi ya muqawama, na leo pia haitafanikiwa kwa vitisho vya kidiplomasia.” Chanzo hicho kiliongeza: “Sharti letu ni wazi; Waziri Mkuu awe huru, asiye tegemezi kwa Marekani, na anayewakilisha vipengele vyote vya nyumba ya taifa ya Iraq.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mchakato wa kuunda serikali mpya ya Iraq umeingia katika hatua nyeti, sambamba na kuongezeka kwa shinikizo la moja kwa moja kutoka Marekani na jumuiya ya kimataifa dhidi ya Baghdad. Hali hii imesababisha sintofahamu ndani ya muungano wa kisiasa unaojulikana kama Mfumo wa Uratibu (Coordination Framework) na kufanya zoezi la kumchagua Waziri Mkuu ajaye kuwa gumu zaidi, hasa kumpata mtu anayeweza kusawazisha matakwa ya ndani ya nchi na mashinikizo ya nje.

Gazeti la Al-Akhbar la Lebanon liliandika kuwa Mark Savaya, mjumbe wa Rais wa Marekani nchini Iraq, katika kauli kali dhidi ya makundi ya muqawama, alidai kuwa uwepo wao uko “nje ya mfumo wa dola”, na kwamba wanachangia “kuleta kuyumba kwa usalama na kudhoofisha uchumi.” Kauli hii imezidi kutatiza mahesabu ya ndani ya Mfumo wa Uratibu na kuifanya hoja ya Waziri Mkuu ajaye kuwa nyeti zaidi. Savaya alisisitiza kuwa: “Hakuna nchi inayoweza kuwa na serikali yenye mafanikio huku kukiwa na makundi ya silaha yanayoshindana na dola.”

Wakati huo huo, viongozi wa Mfumo wa Uratibu katika vikao vyao vya hivi karibuni wameelekeza zaidi mjadala kwenye sifa na vigezo vya Waziri Mkuu badala ya majina ya wagombea. Kuna makubaliano ya awali kwamba Waziri Mkuu ajaye anapaswa kuwa mtu asiye wa msimamo wa mgongano, mwenye uwezo wa kuipa nje ya nchi uhakika, bila kuathiri misingi ya uhuru na mamlaka ya kitaifa ya Iraq. Mohammed al-Fatlawi, mmoja wa viongozi wa muungano huo, alisema: “Wajibu wetu ni kumchagua Waziri Mkuu atakayezingatia mahitaji ya ndani ya nchi na wakati huohuo kudumisha uhusiano wa nje ulio na mizani.”

Hata hivyo, Marekani haijaonekana kuridhika. Joshua Harris, kaimu balozi wa Marekani mjini Baghdad, alisisitiza juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu na kuzuia mashambulizi ya makundi ya muqawama, na hivyo kupanua wigo wa shinikizo hadi katika sekta za nishati na uwekezaji. Wachambuzi wa kisiasa wanaona misimamo hii kuwa ni sehemu ya mkakati mpana wa Washington wa kuipunguza nafasi ya kisiasa na kijamii ya makundi ya muqawama nchini Iraq—mkakati unaotekelezwa si kwa mapambano ya moja kwa moja, bali kwa shinikizo la kisiasa na kiuchumi la hatua kwa hatua.

Kwa upande mwingine, makundi ya muqawama yamekataa vikali madai hayo. Chanzo cha karibu na makundi hayo kilisema: “Muqawama na al-Hashd al-Shaabi pamoja na washirika wao wana angalau viti 97 bungeni, na wao ni sehemu isiyotenganishwa na mlinganyo wa kisiasa wa Iraq. Washington ilishindwa hapo awali kuyadhibiti makundi ya muqawama, na leo pia haitafanikiwa kwa vitisho vya kidiplomasia.” Chanzo hicho kiliongeza: “Sharti letu ni wazi; Waziri Mkuu awe huru, asiye tegemezi kwa Marekani, na anayewakilisha vipengele vyote vya nyumba ya taifa ya Iraq.”

Vyanzo vya kisiasa vinaamini kuwa, licha ya shinikizo la Marekani na msimamo thabiti wa makundi ya muqawama, hali inayotarajiwa zaidi ni kusimamiwa kwa mvutano badala ya mlipuko wa mgogoro. Hii ni kwa sababu pande zote zinafahamu gharama kubwa ya makabiliano ya moja kwa moja, na wakati huohuo zinazingatia athari za kuendelea kwa mvutano wa kikanda katika maamuzi yao.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha